Rekodi
hazidanganyi kwani hadi sasa ni wachezaji watatu tu walioweza kufunga
mfululizo katika mechi tatu za watani wa jadi Simba na Yanga.
Wachezaji
hao ni Kitwana Manara wa Yanga ambaye ni baba mdogo wa Ofisa Habari wa
Simba, Haji Manara, Madaraka Selemani wa Simba na Amissi Tambwe wa
Yanga.
Sasa
ishu ipo hivi, ni Tambwe pekee anayeweza kuvunja rekodi ya kufunga mara
ya nne mfululizo katika mechi hiyo ya watani wa jadi kwani leo anaweza
kuichezea Yanga dhidi ya Simba.
Kitwana
Manara na Madaraka wote wameshaachana na soka la ushindani, hivyo
nafasi ipo kwa Tambwe, raia wa Burundi leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.
Tambwe
alianza kuifunga Simba Septemba 26, 2015 (Simba 0-2 Yanga), Februari
20, 2016 (Yanga 2-0 Simba) na Oktoba Mosi, 2016 ambapo timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1. Katika mechi zote hizo, Tambwe alifunga bao
moja moja.
Kitwana Manara
Machi 30, 1968 (Yanga 1-0 Sunderland)
Juni Mosi, 1968 (Yanga 5-0 Sunderland)
Juni 04, 1972 (Yanga 1-1 Simba)
Madaraka Selemani
Julai 2, 1994 (Simba 4-1 Yanga)
Nov. 2, 1994 (Simba 1-0 Yanga)
Nov. 21, 1994 (Simba 2-0 Yanga)
No comments:
Post a Comment