SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ameonyesha kurudi nyuma katika nia yake ya
kuwapima wabunge kilevi kabla ya kuingia ukumbini, baada ya kukumbushwa
na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, juzi.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Ndugai alisema ataanza
kupima wabunge kilevi pale hali ya matumizi ya vilevi itakapokuwa mbaya
bungeni.
Mei 23, mwaka jana, Spika Ndugai aliieleza Nipashe kuwa kuna wabunge
kadhaa huingia ukumbini wakiwa wametumia vilevi vikali vikiwamo bangi,
viroba na 'unga' hivyo ana mkakati wa kuweka vifaa maalumu vya kupimia
ulevi kwa wabunge wote.
Ndugai alielezea nia hiyo ikiwa ni siku chache tangu aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, afukuzwe kazi na Rais John
Magufuli kwa kujibu swali bungeni akiwa amelewa.
No comments:
Post a Comment