Wednesday, February 15, 2017

SERIKALI KUANIKA ORODHA YA WATUHUMIWA WA USHOGA

Ni tamko kutoka kwa Naibu waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla ambaye ameamua kulifanyia kazi tatizo la mapenzi ya jinsia moja ambalo limekua likilalamikiwa na kwenye mitandao ya kijamii pia.

Naibu waziri amesema “Nikirudi Dar kabla ya kuhamia Dodoma nitaweka wazi orodha ya watuhumiwa wa ushoga wanaojiuza mitandaoni, kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na tutaishinda, nitaendesha operation kamata kamata“

“Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa wa ushoga unaendelea, watakamatwa kimyakimya, wakipatikana watatusaidia wenza wao………… kuna nchi marafiki zinafanya jitihada kupenyeza ushoga Tanzania kudai ni haki ya binadamu kuchagua ampendaye, sisi tunasema NO“

No comments:

Post a Comment