Pamoja
na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali
Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.
Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja
na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major
Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni
Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Tanzania.
Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.
No comments:
Post a Comment