Vita
hiyo juu ya madawa ya kulevya imefika mpaka bungeni na baadhi ya
wabunge walikuwa wakitoa hoja mbalimbali huko mjini Dodoma.
Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga jana alisema yeye yupo tayari kuwataja baadhi ya wabunge wanaohusika na biashara hiyo.
Mbunge
huyo awali alizungumzia mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya elimu
lakini la mwisho aliweza kuzungumzia suala hilo ambalo kwa sasa kila mtu
anataka kutambua nini kinaendelea.
”
Suala ninalotaka ni hili suala linashika headline ni suala la madawa ya
kulevya, naomba niwaambie sisi viongozi naomba niquote, ‘nitasema
ukweli uongo kwangu mwiko.’ Kwahiyo nitakachotaka kukisema mtu yeyote
akitaka anihukumu akihukumu chama changu kwanza, na kama wewe ni mwana
CCM utanichukia rudisha kadi ndo unichukie.
"Wafanya biashara wa madawa ya kulevya hakuna asiowajua, tunawajua humu ndani wapo, nje ya bunge wapo, kwanini hatuwataji?" alihoji.
Aliongeza, “Kwanini
hatuwataji tunakaa kimya? Mheshimiwa mwenyekiti kama kwa ridhaa yako
unaniruhusu mimi nitawataja hata humu ndani. Madawa ya kulevya ni pamoja
na bangi, kuna mbunge alisimama humu alisema bangi hazina madhara
alijuaje kama hazina madhara kama hatumii? tungeanza na huyu.
"Viongozi
wenzangu naomba niwahakikishie kama tutakuwa wanafiki mbinguni sisi
ndiyo tutakaokuwa kuni, tutakuwa kuni mbinguni tunawafumbia macho
watumiaji wa madawa ya kulevya tunakula nao.
"Nimpongeze
ndugu yangu Paul Makonda kwa kuthubutu kutaja neno madawa ya kulevya
lakini nimhakikishie kila marafiki watano wanaomzunguka watatu ni
wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, aanze na hao.”
No comments:
Post a Comment