Thursday, February 16, 2017

MANJI ATHIBITIKA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA, KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Hatimaye imedhibitika kuwa Mwenyekiti wa Timu ya soka ya Yanga na Mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Yusuph Manji anatumia madawa ya kulevya na leo atapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo akiwa pamoja na watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kwa sakata kama hilo.

Katika Kipindi cha michezo katika redio moja nchini Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna,  Simon Sirro amethibitisha kuwa vipimo vya Mkemia Mkuu wa Serikali alivyofanyiwa Manji vinaonyesha kuwa ni Mtumiaji wa Madawa ya kulevya (Hakuyataja aina yake) na kusisitiza kuwa leo mtuhumiwa huyo atapandishiwa kizimbani kujibu shitaka hilo.

Akielezea afya yake tangu alazwe Hospitali, Kamanda Sirro amesema kuwa mwenyekiti huyo wa yanga yuko vizuri na sasa ameruhusiwa kutoka Hospitalini na kurejeshwa mahabusu polisi kusubiri kupandishwa kizimbani.

Sirro amesema kuwa habari kamili kuhusu sakata hilo na watuhumiwa wengine wakiwemo wasanii waliokamatwa zitatolewa leo mbele ya wanahabari Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment