Mwanahabari
nguli Jenerali Ulimwengu, leo anatarajia kuwasilisha maombi Mahakama
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba kuungana na Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe katika kesi ya katiba iliyofunguliwa hivi karibuni.
Ulimwengu
anaomba kuunganishwa katika kesi ya katiba namba 1 ya 2017 kama mdai
dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
“Maombi
ya kumuunganisha yameandaliwa na kesho(leo) yatakuwa mahakamani kuomba
naye awe mdai. Anaomba kujiunga kwa kuwa mambo anayopigania Mbowe naye
ana maslahi nayo kwa sababu ni mambo muhimu ya katiba,” alisema mmoja wa jopo la Mawakili kutoka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya Chadema, Peter Kibatala.
Katika kesi hiyo ya katiba, Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na kukamata.
Mbowe
pia anaomba mahakama itengue vifungu vya 5 &7 vya Sheria ya Tawala
za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki ya katiba.
Mbowe
alifungua kesi hiyo akidai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amekiuka sheria na taratibu katika kushughulikia watuhumiwa wa biashara
ya dawa za kulevya nchini.
Kesi hiyo ya katiba inasikilizwa na majaji watatu, Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday.
Baada
ya kufungua kesi hiyo Mbowe pia aliomba mahakama itoe amri asikamatwe
mpaka maombi yake ya zuio yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Mahakama
ilitoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi kutomkamata Mbowe hadi maombi
yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani yatakaposikilizwa.
Maombi
hayo yalitakiwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki lakini upande wa Jamhuri
ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata uliwasilisha pingamizi,
ukiomba mahakama iyatupilie mbali kwa sababu hana msingi katika
sheria.
Upande
wa mdai ulijibu hoja za kupinga maombi yao na Mahakama ilisikiliza hoja
za pande zote mbili na kupanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Machi 2,
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment