Daimond
ambaye alikuwa ndani ya gari hilo pamoja na mpenzi wake, Zarinah
Hassan, mama yake mzazi na mtoto wake walikuwa wakicheza wimbo mpya wa
Diamond, Marry You aliomshirikika Ne-Yo.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka picha akiwa na Kiongozi wa
Kikosi cha Usalama Barabara, Kamanda Mpinga ambapo amewataka vijana
wenzake kuhakikisha wanachukua tahadhari pindi wanapoendesha magari na
kutumia barabara. Lakini pia ameeleza kuwa amelipa faini kwa mujibu wa
sheria kutokana na kukiuka sheria za usalama barabarani.
“Leo
nilireport kituo kikuu cha polisi wa usalama barabarani kutokana na
Vidoe Clip tuliyopost naendesha gari barabarani bila kufunga mkanda na
pia kuachia usukani na kucheza…. Nikapewa Onyo na Kulipa faini kulingana
ya Mujibu wa sheria… tafadhali watanzania na Vijana wenzangu…
tuhakikishe tunafunga mikanda pindi tupandapo na tuendeshapo Magari
Maana ni Hatari kwa Maisha yetu na inaweza kukupeleka kunyea debe
pia…🙏” ameandika Diamond
No comments:
Post a Comment