Mtu
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kosa la
kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha
pinchi 240 na ndonga mbili.
Taarifa
ya jeshi hilo iliyotolewa leo, imedai kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa
jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43, amekamatwa majira ya
saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba
wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza
Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi
walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya
madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja
na uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo.
Aidha
wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za
mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa
kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa
madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.
Tukio lilivyokuwa
Askari
walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo, ndipo
ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi nyumbani
anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia
dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogovidogo
maarufu kama pichi.
Wakati
askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa alishtuka na
kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza ushahidi.
Aidha
askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na baadhi YA askari
waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni lakini
bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la
choo.
Msangi
amesema wakati huohuo askari wengine waliokuwa nje walikwenda kuvunja
bomba linalopitisha uchafu/choo linalokwenda kwenye shimo na kuweka
kizuizi hapo na kufanikiwa kupata ndonga 2 za dawa za kulevya huku
nyingine zikibebwa na maji .
Polisi
wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa
watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya madawa ya
kulevya.
No comments:
Post a Comment