Monday, July 31, 2017

CRISTIANO RONALDO KUPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Ile kesi inayomhusu mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuhusu masuala ya kodi inachukua sura mpya hii leo ambapo mwanandinga huyo atapanda kizimbani kwa mara ya kwanza kusomewa mashtaka yake.

Ronaldo ambaye ni mwanamichezo anayeingiza pesa nyingi zaidi duniani anadaiwa kukwepa kiasi cha kodi cha  £14.7m kuanzia mwaka 2010 ikiwa ni mwaka mmoja tu toka ajiunge na Real Madrid kutoka Manchester United.

Ronaldo kabla ya kupandishwa mahakamani alishajitokeza hadharani na kusema hana mashaka hata kidogo kuhusu kesi yake kwani kila kitu kiko wazi na kwa kuwa hana kosa baasi hana cha kuogopa.

Kesi inayomkabili Cristiano Ronaldo ilishawahi kumtokea Lioneil Messi ambapo mahakama ilimhukumu mieI 21 nje ya jela lakini baadae mahakama ikamuamuru alipe £252,000 ili kuepuka adhabu hiyo.

Lakini tofauti ya kiasi cha kodi alichokwepa Ronaldo na aliyokwepa Messi ni tofauti sana kwani Messi alikwepa kulipa £4m tu huku Ronaldo akikwepa £14m ikiwa ni tofauti ya karibia £10m.

Endapo Ronaldo atapatikana na hatia ni wazi kwamba atapewa adhabu kubwa kuliko ya Lioneil Messi. Kesi hii inamnyima raha sana Ronaldo na iliwahi kumfanya atake kuihama Real Madrid.

No comments:

Post a Comment