Thursday, July 26, 2018

MBARAWA AWAPA WAKANDARASI NJIA ZA KUFUATA ILI WALIPWE MALIPO YAO

Waziri wa maji na umwagiliaji , Profesa Makame Mbarawa,amewataka wakandarasi wote nchini ambao wanatekeleza miradi ya maji kupeleka vibali vyao vya malipo sehemu waliyoingia nayo mkataba ya kazi  ili vibali hivyo viweze kupelekwa wizarani waweze kulipwa fedha zao wanazodai mamlaka za maji husika.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo mara baada ya kulalamikiwa na mkandarasi wa kampuni ya Lugoba Stones anaejenga mradi wa maji wa Kilwa Masoko unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira  Mjini Lindi, LUWASA ambao anawadai mamlaka hiyo shilingi milioni miamoja na nane huku waziri akimuomba mkandarasi huyo kuendelea na kazi sehemu iliyobakia ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya maji na fedha anayodai atalipwa bila matatizo yoyote.

Kwa upande mwenyekiti wa mamlaka wa mji mdogo kwa Kilwa masoko, Ismai Silim, akaishukuru serikali ya awamu ya tano jinsi inavyotekeleza miradi yake ya maji ambayo italeta manufaa kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment