Na James Timber, Mwanza
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imepiga marufuku Wadau mbalimbali na Viongozi wa Idara ya Elimu kuwafokea na kuwatukana walimu, lengo likiwa kuboresha elimu kwa wote.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Juma la Elimu Ki Wilaya katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mkuu wa Wilaya wa Nyamagana Merry Tesha, amesema kuwa katika kuboresha elimu lazima mwalimu awe rafiki wa viongozi na asihishi kwa hofu.
"Nimepokea malalamiko kuwa kuna baadhi ya viongozi wakifika kwa ajili ya ziara wanafika na kuwafokea walumu jambo linalochangia walimu kuwa na hofu mpaka wanafundisha chini ya kiwango," alisema
Pia aliwataka walimu kuwafundisha wanafunzi wawe wajanja kwa lengo la kuepuka tatizo la mimba mashuleni na ikitokea wamepata ujauzito wazazi na walimu wafuatilie sambamba na adhabu itolewe kama fundisho kwa wengine.
Tesha amesema kuwa kumekuepo na malalamiko kuwa walimu wa Shule ya Msingi wanapeleka wanafunzi kidato cha kwanza hawajui kusoma na kuandika, huku akiwata wazazi wahakikishe wanafuatilia maendeleo ya watoto mashuleni kwa kushirikiana na walimu.
Aidha amesema kuwa Nyamagana inaweza kuondoa "zero" kama walimu watakuwa na mazingira mazuri ya kufundishia, huku akiipongeza Idara ya Ukaguzi kwa kazi nzuri wanayofanya huku akisisitiza kaulimbiu ya mwaka huu isemayo "Uwajibikaji wa Pamoja kwa Elimu Bora kwa Wote"

No comments:
Post a Comment