Thursday, May 17, 2018

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI KOMBE LA DUNIA URUSI

Mashindano ya Kombe la dunia la watoto wa mitaani chini ya shirika la Steet Child United na udhaamini wa makampuni na taasisi tofauti, zaidi kampuni ya mawasiliano ya simu ya nchini Urusi, Megafon yamefikia tamati leo kwa kuchezwa mechi za mshindi wa tatu na fainali kwa watoto wa kike na wakiume, ambapo timu ya Tanzania (wasichana) iliweza kuwa mshindi wa pili baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka Brazil, baada ya kutokea mawasiliano mabaya kati ya mlinzi wa Tanzania na mlinda mlango wake katika hatua za mwisho za mchezo huo.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa aina yake, huku Brazil wakimiliki mchezo sana na kufanikiwa kumficha kiungo mkuu wa Tanzania, Nahodha Asteria Robert na hapo Tanzania ikawa ishadhibitiwa. Kipindi cha pili Tanzania kidogo walicheza vizuri lakini hawakurudisha goli hilo.
Kipindi cha kwanza Tanzania walicheza kwa presha sana na hawakutulia na mpira na hali hio ikawapotezea kujiamini. Lakini mwisho wa siku asiekubali kushidwa sio mshindani. Tanzania ikashika nafasi ya pili katika mashindano hayo kwa wanawake.

Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na watu wengi mashuhuri, wakiwemo viongozi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi pamoja na mchezaji wa zamani wa Arsenal na bingwa wa kombe la dunia kwa kikosi cha Brazil na kiungo maarufu na mwenye uwezo wa viwango vya dunia, Gilberto Da Silva.

Timu zote baada ya mechi zilipata nafasi ya kumuuliza swali moja Gilberto Da Silva. Tanzania iliuliza swali kupitia Nahodha wake, Asteria Robert kwa Kiswahili na mkalimani Mohamed Masour Nassor akatafsiri moja kwa moja kwa lugha ya Kireno ya mchezaji huyo. Swali hilo lilikua hivi,"Je ni vipi Unawasaidia watoto wa mitaani kufikia ndoto zao na wale watoto ambao wanataka kuwa wachezaji wa viwango vya dunia kama wewe? Mwisho ikafuata sherehe ya ufungaji wa mashindano hayo.

Muda wa zawadi ulipofika, Tanzania ilizawadiwa Kombe na medali za shaba kwa kila mchezaji na viongozi wa timu kutoka chama cha mpira cha Urusi na zawadi zengine kutoka kwa chuo cha Patrice Lumumba. Tanzania pia ilitoa kiungo bora wa mashindano ambae ni nahodha, Asteria Robert ambae kwa kweli alistahili sana. Kwa upande wa bingwa wa wanaume ni Timu  ya Uzbekistan baada ya kuilaza kwa mikwaju ya penati timu ya Pakistan.

No comments:

Post a Comment