RAIS John Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na mabalozi kushindwa kutekeleza maagizo aliyowapa na kusema balozi atakayeshindwa kuonyesha ufanisi atarudishwa nyumbani ili kazi hiyo wapangiwe watu wenye uwezo.
Aliyasema hayo jana Ikulu Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha, Alphayo Kidata kuwa Balozi wa Canada na Msalika Makungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora.
Balozi Kidata pia ataiwakilisha nchi ya Cuba akichukua nafasi iliyoachwa na Balozi Jack Zoka ambaye amemaliza muda wake.Makungu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Thea Ntara ambaye amestaafu.
Rais Magufuli alisema alitoa maagizo mabalozi wote wampe taarifa juu ya utendaji kazi na manufaa ambayo nchi imeyapata kwa uwepo wa kila Balozi katika nchi aliyopangiwa kila robo mwaka, lakini hawafanyi hivyo.
"Nataka nijue katika kipindi ambacho Balozi ameteuliwa kuiwakilisha Tanzania nchi fulani, tumenufaikaje na uwepo wake kwenye nchi ile," alisema Rais Magufuli na kueleza zaidi:
"Kuteuliwa sawa, lakini siyo lazima ukae katika ubalozi huo kwa kipindi chote ulichopangiwa.
"Ukishindwa kuleta manufaa unarudishwa na huko anapangiwa mtu mwingine atayeleta manufaa kwa nchi."Rais Magufuli alitaka mabalozi kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa manufaa ya taifa na kutoa taarifa ya wanachofanya.
KAZI NZURI
Katika hatua nyingine, akizungumza katika hafla hiyo, Rais Magufuli aliipongeza Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kufanya kazi nzuri katika sekta ya elimu na afya.
Pia Rais Magufuli alieleza kutoridhishwa na utendaji katika sekta za maji na ardhi kutokana na usimamizi mbaya wa miradi mingi ya maji na usimamizi mbaya wa masuala ya ardhi na mipango miji.
Alisema tangu mwaka 2010 serikali imetoa Sh. bilioni 109 kwa ajili ya miradi ya maji katika maeneo mbalimbali, lakini uchunguzi umeonyesha miradi iliyotekelezwa ipasavyo na kuonesha thamani halisi ya fedha zilizotumika ni ya Sh. bilioni 17 tu.
Kutokana na hali hiyo, Rais Magufuli aliagiza wataalamu wote wa idara za maji katika halmashauri zote wasimamiwe moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Aidha, Rais Magufuli aliagiza wataalamu wa ardhi na mipango miji katika halmashauri zote nchini wasimamiwe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Alisema lengo la maagizo hayo ni kuimarisha usimamizi wa shughuli zinazofanywa na idara hizo na kuwawajibisha wahusika pale mradi unapotekelezwa chini ya kiwango.
"Sasa hivi kila mahali watu wanalalamikia maji, wabunge wanalalamika, wananchi wanalalamika, serikali imetoa fedha lakini miradi haitoi maji," alisema, "na ukichunguza miradi hii inasimamiwa na wahandisi wa maji wa halmashauri ambao Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ambaye ana wataalamu wa maji hana uwezo wa kuwawajibisha.
"Wahandisi wanawajibika kwa madiwani, sasa hatuwezi kwenda kwa mtindo huo."
Kadhalika, Rais Magufuli alisema kwenye ardhi kuna matatizo mengi na mipango miji kwani watu wanadhulumiwa ardhi, ugawaji wa viwanja ni matatizo, maafisa ardhi na mipango miji wanachelewesha vibali vya ujenzi.
"Huku nako Katibu Mkuu wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi hana mamlaka ya kuwachukulia hatua, (na) hili nalo ni tatizo." Rais Magufuli alimtaka Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo kukutana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwele na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kutengeneza muundo utakaozingatia maelekezo hayo.

No comments:
Post a Comment