Thursday, March 15, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAOMBA WATANZANIA KUWA WATULIVU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali na kuacha kufanya mambo yasiyokuwa na tija katika uchumi na maisha ya kila siku.

Majaliwa ameyasema hayo mjini Dodoma katika uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha Standard Gauge kutokea Morogoro mpaka Makotopora, ambapo Waziri Majaliwa aliwasihi Watanzania kuwa watulivu kusubiri utekelezaji.

“Nawasihi Watanzania wote kuwa watulivu kusubiri utekelezaji lakini kushiriki kikamilifu katika kujenga ujenzi wa miundombinu hii ili tuweze kupata manufaa. Nataka niwasihi Watanzania nikianza na hii reli yetu, reli hii ni fursa kwetu sote tunaopitiwa na reli hii kutoka Dar, Mwanza, Kigoma kupitia hapa Dodoma na Mh. Mbunge ameeleza kwa wana Dodoma mimi nipanue wigo kwa wote wanaopitiwa na reli hii tuitumie kama fursa ya kukuza uchumi wetu kwa mtu mmoja mmoja,” amesema Waziri Majaliwa.

“Ndugu Watanzania nataka niendelee kuwasihi tuachane na mambo ambayo hayana tija kwa uchumi wetu na kwenye maisha yetu ya kila siku tuendelee kuhamasishana kuunga mkono shughuli za maendeleo kila mmoja ajitoe kuunga mkono jitihada za serikali.”

No comments:

Post a Comment