Wednesday, September 20, 2017

MGODI WA TANZANITE KULINDWA NA JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza Jeshi la Wananchi kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta mkubwa kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite na kuweka mitambo maalum, ili kulinda madini hayo yasiendelee kuibiwa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambako ameende kuzindua barabara ya lami iliyojengwa kwa bilioni 32.5 ya KIA- Manyara, na kusema kwamba ni lazima ulinzi huo uwekwe ili kuokoa rasilimali za Tanzania zisiendelee kuibiwa na nchi kubaki masikini.
"Eneo la Simanjiro kuanzia Block A mpaka Bolock D ambalo lina madini mengi, ninaagiza Jeshi la wananchi likishirikiana na Suma JKT, waanze kulijengea ukuta eneo lote, wataweka fensi juu na wataweka camera, patawekwa mlango mmoja na itawekwa mitambo maalum, hata kama utameza Tanzanite itaonekana, hata ukificha kwenye kiatu itaonekana", amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli atakuwepo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 3, ambapo pia atatoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Septemba 23, 201

No comments:

Post a Comment