Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Ndg. Humphrey Polepole amesema sababu kubwa ya vijana wa Mbeya kuonekana kuyumba ni kutokana na kunyimwa nafasi za kuwa viongozi.
Akiwa Mkoani Mbeya kwenye ziara, Polepole ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wanachama wa CCM ambapo amesema kwamba watu wa Mbeya wamekuwa wakishindwa kuwapatia vijana uongozi ndiyo maana wameyumba kitu ambacho ni makosa kwani dunia nzima vijana wanapaswa kupewa uongozi.
Polepole amesema wao kama CCM wanataka kuwasaidia vijana hao kwa sababu ndicho chama ambacho ni sauti ya wanyonge, wasio na uwezo pamoja na wafanyabiashara ndogondogo
Aidha Polepole ameongeza kwamba "Tuchuke maoni yao tuielekeze serikali ikatatue na kisha tuiangalie serikali inafanya nini kisha tupeleke na kuzisema sifa za serikali na kazi ambazo zinafanywa na serikali yetu. Wananchi watatupenda," Polepole.
Pamoja na hayo kiongozi huyo amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinapaswa kuwa Chama kinachotoa majibu papo kwa hapo kwa wananchi wake.

No comments:
Post a Comment