Dar es Salaam. Baada ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Dart) kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, baadhi ya magari madogo, daladala na bodaboda wametumia fursa hiyo kupitisha magari yao katika barabara zinazotumika na magari hayo.
Mwananchi limeshuhudia daladala zikipita katika vituo hivyo huku zikishusha na kupakiza abiria katika kila kituo cha mwendokasi, huku trafiki wakielekeza baadhi ya magari kutoka kwenye barabara hizo.
Hata hivyo vituo vingi vya mwendokasi vimefungwa isipokuwa kituo cha Ubungo ambacho wahudumu wameonekana wamelala huku kukiwa hakuna abiria wanaoingia katika kituo hicho.
Dereva wa daladala linalofanya safari zake Mbagala Rangitatu - Simu 2000 Jafari Himid amesema kutokana na foleni iliyopo katika barabara hiyo, wameamua kutumia barabara za mwendokasi ili kuokoa muda.
"Bila kufanya hivi hatuwezi kuwahisha abiria na hizi barabara leo hazina matumizi, hata trafiki wanatuachia hawajatukamata," amesema Jafari.
Hata hivyo barabara ya Morogoro Road ina foleni kubwa inayosababishwa na kipande cha barabara ya jangwani kujaa tope.
No comments:
Post a Comment