Mbunge
wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Peter Msigwa amefunguka na kudai
nchi ya Tanzania imefika mahali pa hovyo kutokana na watawala kuiendesha
nchi kwa mtazamo wao na sio kufuata sheria na kanuni zilizopo.
Msigwa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akimuombea ridhaa mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu ili aweze kupata kura za ndio kwa wananchi hao siku ya kupiga kura ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa , huku akisindikizwa na mameya na Wabunge mbalimbali kutoka UKAWA.
"Watawala
wanaendesha nchi kwa 'personality' na badala ya sheria na kanuni. Kwa
bahati mbaya sana wale ambao wanategemewa kusema, kukemea pamoja na
kuonya wamekaa kimya. Lakini baadhi yetu tumeamua iwe mvua, jua, iwe
mabomu ya polisi, vituo vya polisi hata gereza tutazungumza hatutoogopa
mtu yeyote", alisema Msigwa.
Pamoja
na hayo, Msigwa aliendelea kwa kusema "nchi ya Tanzania imefika mahali
ambako kiongozi hawezi kusemwa, Mkuu wa Mkoa hata Spika wa Bunge".
Kwa
upande mwingine, Msigwa aliwaambia wananchi wa Jimbo la Kinondoni
kwamba wakimuona Mbunge anajikomba komba serikalini basi watambue mtu
huyo hatambui wajibu wake anaopaswa kuutekeleza au kuufanya.
No comments:
Post a Comment