Baada ya Simba kushinda kwa magoli 4-0 kwenye mcheO wao wa kwanza wa
kimataifa dhidi ya Gendarmerie, mashabiki wa wekundu wa Msimbazi
wanasema Simba ilikuwa na uwezo wa kupata ushindi mkubwa zaidi ya
walioupata kutokana na udhaifu wa wapinzani wao.
Kocha msaidizi wa Sima Masoud Djuma amesema waliwataka wachezaji
wasitumie nguvu kubwa kwenye mchezo mmoja kutokana na kukabiliwa na
michezo miwili ya VPL hivi karibuni.
“Nimemsikia mwalimu wao anasema zamani walikuwa wanafungwa hadi magoli
tisa au 10, huo ni mpira wa zamani, mpira wa kisasa kitu cha muhimu ni
kwamba hatukuruhusu kufungwa goli.”
“Halafu sisi tuna mechi mbili za ligi zimeongozana hapa karibu kwa hiyo
ilikuwa lazima tucheze kwa mpangilio kwa sababu ni lazima tushinde zote
kwa hiyo hatukutumia nguvu nyingi kwenye mchezo mmoja.”
No comments:
Post a Comment