Monday, October 9, 2017

UTURUKI NA MAREKANI KATIKA MZOZO WA UTOAJI VISA

Turkish and US flags. File photo
Uturuki na Marekani wamekuwa kwenye mzozo wa kibalozi ambapo huduma kadha za visa zimesitishwa.
Ubalozi wa Uturuki mjini Washington ulisema kuwa ulitaka kutathmini kujitolea kwa serikali ya Marekani kwa usalama wa ubalozi wake na wafanyakazi wake.
Taarifa kama hiyo ilikuwa imetolewa mapema na ubalozi wa Marekani mjini Ankara.Hii inajiri baada ya mfanyakazi wa ubalozi wa Marekani mjini Instabul kushikwa wiki iliyopita, kwa kushukiwa kuwa na uhusiano na kiongozi wa dini anayedaiwa kuhusika kwenye jaribio la mapinduzi lililofeli mwaka uliopita nchini Uturuki.
Marekani ililaani hatua hiyo kuwa isiyo na msingi na inayohujumu uhusiano kati ya nchi hizo.Fethullah Gulen. File photoMfanyakazi aliyekamatwa alikuwa ni mwanamume raia wa Uturuki.
Ubalozi wa Marekani ulisema kuwa huduma za visa zisizo za kuhamia Marekani nchini Uturuki zimesitishwa.
Visa zisizokuwa za kuhamia kabisa Marekani ni kama zile za kitalii, za kutafuta matibabu, za kibiashara na ajira ya muda na masomo.Wale wanaotaka uraia au kuishi Marekani huomba visa za kuhamia Marekani.
Uturuki kwa miezi mingi imekuwa ikiishinikiza Marekana kumsalimisha kiongozi wa dini Fethullah Gulen, kwa madai ya kuhusika kwenye jaribio la mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2016.

No comments:

Post a Comment