MBWANA SAMATTA.
Taifa Stars inaumana na Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo unaotambulika katika kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Samatta aliambia Nipashe jana kwenye mazoezi ya asubuhi kuwa mchezo wa leo ni muhimu katika harakati zao za kutaka kupanda kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na FIFA.
“Hiki ni kipimo kizuri kwetu, ni vyema kuanza na timu ambazo hatujapishana nazo sana kabla ya kufikiria kucheza na timu kubwa zaidi, tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa sababu hii ni timu yao..,timu ya Watanzania wote,” alisema Samatta.
Naye Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga, alisema anawategemea washambuliaji Samatta na Simon Msuva kuongoza mashambuliaji ya "kuiangamiza" Malawi huku safu ya ulinzi ikiwa chini ya beki wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda.
Mayanga alisema pia uwepo wa nyota wengine wa ndani , Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu na Himid Mao inampa nafasi kubwa taifa Stars kufanya vizuri leo.
Taifa Stars ipo katika nafasi 125 kwenye viwango vya ubora vya FIFA vilivyotolewa Septemba 14 huku wapinzani wao Malawi wakiwa juu kwa nafasi tisa zaidi, wanashika nafasi ya 116.
Malawi imeporomoka kwa nafasi 10 ukilinganisha na viwango vya mwezi Julai ambapo walikuwa katika nafasi 106 huku Taifa Stars yenyewe ikishuka kwa nafasi tano (ilikuwa katika nafasi ya 120).
No comments:
Post a Comment