Akizungumza na gazeti hili jana, Samatta alisema pamoja na kuwa Yondani hajaitwa kwa muda mrefu kwenye timu hiyo, kurejea kwake kumeongeza uimara katika safu yao ya ulinzi.
Kwa kweli Yondani amerejea na kiwango kikubwa na uwapo wake unaifanya safu yetu ya ulinzi kuimarika zaidi, lakini pia uwezo ulioonyeshwa na Msuva unatupa mwanga kuwa kama tutakuwa na wachezaji wengi wa aina yake tunaweza kufanya vizuri zaidi,” alisema Samatta.
Katika mchezo wa kirafiki uliochezwa juzi dhidi ya Botswana, Msuva alifunga mabao yote mawili na kuipa Taifa Stars ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo huo ulipo katika Kalenda ya FIFA.
Samatta, alisema Msuva ameonyesha kiwango kikubwa na kumtabiria kufika mbali zaidi kwenye timu yake mpya anayoichezea kwa sasa.
Msuva kwa sasa anaichezea klabu ya Difaa Hassan El Jadidi (DHJ FC) ya nchini Morocco aliyojiunga nayo akitokea kwa mabingwa wa soka Tanzania, Yanga.
No comments:
Post a Comment