Tuesday, September 5, 2017

NDUGAI:MLISEMA SPIKA DHAIFU SASA MTAKOMA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai

Mara baada ya kikao cha kwanza kwenye mkutano wa 8, wa Bunge la 11, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai amesema wale waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi, sasa wataona dhahiri udhaifu wake uko wapi.

Spika Ndugai ameeleza hayo wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

“Taratibu zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu, nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako maneno kama haya hayana umuhimu”, alisema Spika Ndugai.

Samabamba na hilo, Spika Ndugai aliwakaribisha wabunge walioapishwa huku akiwafunda wabunge wengine, kwamba kiapo walichokula wenzao leo kiwa kumbushe utii na uaminifu kwa kwa tiba ya nchi.

“Kiapo hiki cha uaminifu kina tukumbusha wengine ambao tuliapa utii wa Katiba na kiapo chetu kwa ujumla wake, kuhusiana na uaminifu na utii.  Ni vizuri kuisoma Katiba na kuipitia ili uweze kujua nafasi ya vyama vya siasa na uhusiano wa mbunge na chama cha siasa”, alisisitiza Spika Ndugai.

Wabunge hao walioapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati na kuanza kazi mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment