Wednesday, September 6, 2017

KIPINDUPINDU CHAENEA KWA KASI NIGERIA

Mamia ya watu wanasumbuliwa na ugonjwa huo

Umoja wa mataifa umesema kwamba ugonjwa wa kipindupindu umeendea kwa kasi kubwa katika kambi za makaazi ya watu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Inasemekana kwamba zaidi ya matukio 530 ya ugonjwa huo yameripotiwa katika jimbo la Borno, ikiwa ni mara tatu zaidi ya idadi iliyotolewa siku tano zilizopita.

Zaidi ya watu ishirini wamefariki dunia. Mapigano kati ya vikosi vya serikali na Boko Hamam, yamesababisha watu zaidi ya milioni mbili kuyahama makazi yao.

No comments:

Post a Comment