Wednesday, September 6, 2017

KINGEREZA NOMA HAMORAPA KUJIFUNZA PRIVATE

Harmorapa.

BWA’MDOGO asiyekaukiwa matukio, Harmorapa anatarajia kuanza kujinoa katika suala zima la Lugha ya Kingereza kwa mtaalam wa kufundisha lugha hiyo, James Mramba ‘Mr. English’.

Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kuona kuna fursa anaikosa katika suala zima la kuwasiliana na wafanyabiashara mbalimbali hususan atakapokwenda kupiga shoo nje ya nchi.

“Nimeamua kujifunza Kingereza na sehemu sahihi kwangu ni kwa Mr. English kwa sababu anatoa huduma za mobile.

Atanifuata nyumbani, najifunza private,” alisema Harmorapa. 

No comments:

Post a Comment