An overturned vehicle on a flooded street in Miami
Zaidi ya nyumba milioni 3.4 katika jimbo la Florida hazina nguvu za umeme na sehemu za mji wa Miami zimefurika maji.
Vifo vitatu vinavyotokana na kimbunga hicho vimeripotiwa wakati Irma kikielekea sehemu za kaskazini.
Kituo cha vimbunga cha Marekani kinasema Irma kimesababisha upepo sehemu tofauti za katikati mwa Florida.
Mapema kimbunga hicho kilipiga maeneo yanayozunguka mji wa Fort Myers.
Irma tayari kimeharibu sehemu za Caribbean na kuya takriban watu 28.
Watu milioni 6.3 huko Florida wameambiwa wahame.
No comments:
Post a Comment