Papaa Msoffe na wenzake, Alex Machari (Alex Massawe) na Kapteni Makongoro Nyerere, walifungua maombi mahakamani hapo wakiomba kibali cha kukata rufaa Mahakama ya Rufani nje ya muda kupinga hukumu na amri ya Mahakama, kumuondolea umiliki wa nyumba hiyo kutokana na kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mfanyabiashara wa madini, Onesphory Kituly.
Papaa Msoffe alikuwa akidai kuwa nyumba hiyo ni mali yake na kwamba aliinunua kutoka kwa Alex Massawe.
Desemba 23, 2015, Mahakama ya Ardhi ilimnyang’anya Papaa Msoffe umiliki wa nyumba hiyo, kutokana na kesi ya msingi ya mgogoro wa umiliki iliyofunguliwa na Kituly, kabla ya kuuawa.
Mjibu maombi, Bryson Kituly ambaye ni mwakilishi wa marehemu Kituly, kupitia kwa Wakili Stock Joachim aliweka pingamizi, akiiomba mahakama iyatupilie mbali maombi hayo akidai siyo halali kwa kuwa watoa maombi wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi kinachoipa Mahakama mamlaka ya kusikiliza maombi hayo.
Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Crecencia Makuru alisema kutumia vifungu vingi vya sheria kufungua maombi, kikiwamo kifungu sahihi na kisicho sahihi inamaanisha watoa maombi hawana uhakika na wanachotaka Mahakama iwafanyie.
No comments:
Post a Comment