Chid Benz ameeleza hayo kupitia kipindi cha 'Friday Night Live' (FNL), kinachorushwa na EATV pamoja na EA Radio baada ya siku kadhaa kupita tokea alipofanyiwa 'interview' na eNewz na kudai ana kolabo na 2pac, jambo ambalo watu wengi waliamini msanii huyo ameanza kuharibikiwa akili kutokana na dawa za kulevya na kupelekea Madee kutoa maoni yake binafsi kwa kudai ni bora yeye ambaye havuti hata sigara.
"Unaweza ukawa huvuti hata sigara lakini ukawa mbea, kwa sababu Madee watu tumnajua kama ni mbea na mnafki maana anapenda kuninanga, anahisi labda mimi ipo siku nitafanya kitu", alisema Chid Benz.
Pamoja na hayo Chid Benz aliendelea kwa kusema "mtu kama anaku-post kitu katika mitandao ya kijamii halafu chini yake anakuandikia 'ndiyo maana mimi sivuti hata sigara' 'that means' anaonyeshea watu kwamba kuna kitu Chid Benz anatumia au anavuta ndiyo maana yeye hatumii sigara kwa hiyo mimi amenitengenezea ubaya mpaka kupelekea watu ku-comment kwamba madawa yamenisababisha nichanganikiwe", alisisitiza Chid Benz
No comments:
Post a Comment