Mfanyabiashara maarufu na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi amekuwa miongoni mwa watu wakubwa ambao wanafuatilia kwa ukaribu uchaguzi huo huku akiombea upite kwa amani tofauti na ule uliotokea miaka minne iliyopita.
Mengi amethibitisha hilo kupitia mtandao wake wa Twitter kwa kuandika, “This is a historical election for Kenya. A peaceful election is victory not just for Kenyans but all East Africans.@UKenyatta @RailaOdinga.”
Katika uchaguzi huo vita kubwa ya kuwania kiti cha urais ipo kwa Uhuru Kenyatta ambaye anawakilisha chama cha Jubilee Party na Raila Odinga ambaye anawania kupitia umoja wa NASA
No comments:
Post a Comment