Wednesday, August 9, 2017

RC MAKONDA AAGIZA CV ZA WATENDAJI KATA DSM KUPIWA UPYA

 
Hatua hiyo imefuata baada ya Mkuu huyo wa Mkoa Dsm kufika katika eneo la Bunju B jijini humo kwa maelekezo ya Rais Magufuli aliyetoa siku 4 kutatuliwa kero za eneo hilo.

Jana Katika mkutano na wananchi wa eneo hilo, RC Makonda alilazimika kumuinua mtendaji wa kata hiyo na ndipo alipogundua wengi wao hawaelewi vizuri majukumu yao na ndipo alipomuagiza mkuu wa Wilaya ya Kindondoni Ally Happi kukagua Cv za watendaji wake wa kata na mitaa mara moja ili ajue nani.
RC Makonda amedai Watendaji hao kutoelewa majukumu yao ndio imekuwa sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero ndogondogo na hatimaye Wanasubiri Rais akipita wanamsimamisha kwa matatizo madogo madogo yakiwemo ya Vyoo, Umeme na masoko. 
Juzi Wakati Rais Magufuli anarejea Jijini Dsm kutoka Mkoani Tanga alikokuwa kwenye ziara yake ya siku tano, alisimamishwa na wananchi wa Bunju B katika wilaya ya Kinondoni na kumueleza kero zao na baada ya hapo Rais Magufuli alitoa agizo la ndani ya siku nne Mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda awe amefika na kutoa majibu ya kero hizo.

No comments:

Post a Comment