Mshambuliaji wa kimataifa huyo, Okwi alitua jana usiku jijini Dar es Salaam akifuatana na Kiungo wa Haruna Niyonzima pamoja na mfungaji bora wa ligi kuu Ghana Nicholas Gyan ambao wote wamekuja kuungana na wachezaji wenzao ili kuongeza nguvu kwenye Tamasha la hilo ambalo watatambulishwa rasmi.
Mara baada ya kuwasili wachezaji hao, Afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara amesema "Yes Haruna 'in the house', Gyan ndani, Okwi ameshatua. Sijui unakosaje kesho, this is Simba ukinuna saga chupa". amesema Manara kupitia Instagram yake.
Kwa upande mwingine, mechi ya kesho itakuwa ya tatu kuchezwa na simba kujiandaa kuelekea michuano ya Ligi kuu huku wakiwa wamepoteza mechi moja wakifungwa na timu ya Orlando Pirate bao 1-0 na nyingine kutoka sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Bidvest FC zote wamechezea nchini Afrika ya kusini walipokuwa wameenda kuweka kambi ya maalum ya maandalizi msimu mpya.
No comments:
Post a Comment