“Nimerudi kwa Mungu wangu ili mambo yangu yaende vizuri maana tunafanya muziki wa dunia anatusamehe ila kurudi kwake pia ni jambo la kawaida sana,” amesema Nuh.
Pia msanii huyo amekanusha taarifa zilizotolewa na aliyekuwa mke wake kuwa ameacha kumjali mtoto wake Anyagile tangu watenganae na kusema tuhuma hizo hazina ukweli.
“Mara ya mwisho nilikuwa na Anyagile kwenye photoshoot ya ngoma yangu mpya jana kwa Mx Carter, inayotoka hivi karibuni sasa yeye anavyosema sijamuona mtoto muda mrefu sijui anamaanisha nini, ” amesema Nuh.
Pia ameongeza kuwa “Anaongea vibaya kwenye media sio vizuri, mimi na fan base yeye mwanamke anatakiwa ajue anaongea nini, ila muache aongee akikua ataacha, vile vile mimi sina tatizo naye kama kaolewa, yeye si ndio kaamau mimi bado kijana na kila mtu anafanya anachotaka mimi nimemrudia mungu huwezi jua atanipatia mke mwingine mwema”.
No comments:
Post a Comment