Friday, August 4, 2017

KINANA AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KUKSOA AWAMU ZILIZOPITA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana amefunguka na kusema kuwa anachofanya Rais Magufuli ni sawa kwani yeye ana sahihisha makosa ambayo yalifanywa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliopita.

Kinana amesema hayo jana alipokuwa akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Mkanyageni wilayani Muheza katika ziara ya kikazi ya Rais Magufuli mkoani Tanga iliyoanza jana  mpaka siku ya Jumamosi ambapo Rais ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Chongoleani Tanga.

"Yako maneno yanayosema kwamba wakati mwingine Rais Magufuli ni mkali, wakati mwingine wanasema Rais anakosoa awamu zilizopita, awamu zote zilizopita ni za CCM awamu hii ni ya CCM kama kuna kasoro, au kama kuna mambo awamu zilizopita hayakwenda vizuri awamu hii ya CCM chini ya Magufuli kukosoa au kusahihisha yale yaliyoharibika huko nyuma si dhambi. Aliyeharibu Mwana CCM, anayekosoa mwana CCM na anayesahihisha ni mwana CCM tuache kulalamika tuchape kazi" alisema Kinana

Mbali na hilo Kinana amesema wanachotaka wananchi ni maendeleo na ndiyo kitu ambacho Rais Magufuli anafanya sasa na kudai yeye anatimiza mahitaji ya wananchi na kufanya yale mambo ambayo viongozi wengine walikuwa hawafanyi. 

No comments:

Post a Comment