Kusemekana kwa soko la uhakika na kuporomoka kwa bei ya mbaazi kumesababisha vilio kutoka kwa wakulima wa zao hilo wilayani Nachingwea.
Wakizungumza na Muungwana kwa nyakati na maeneo tofauti wiki hii, baadhi ya wakulima walisema hawaelewi watazifanyia nini baada ya kuvuna. Huku wengine wakiapa kutovuna.
Mkulima aliyejitambulisha kwa jina la Manyangu Nzige, alisema haelewi atazifanyia nini baada ya bei ya zao hilo kuwa ndogo, isiyolingana na gharama za uendeshaji.Huku akiweka wazi kuwa itakuwa ni vigumu kuvuna mbaazi zote bila kuweka vibarua wakumsaidia. Hata hivyo kilo moja inanunuliwa kwa shilingi 250. Hivyo ni dhahiri atapoteza fedha kuweka vibarua kwa bei hiyo.
Alisema ingawa mbaazi ni zao la chakula, lakini baada ya kuhamasishwa na serikali walime mazao mbadala wa korosho, walilitupia jicho zao hilo kwa kuwekeza fedha nyingi katika kilimo cha zao hilo na kulifanya ni zao la biashara.
"Ingawa tunaambiwa mbaazi ni mboga, lakini tulihamasishwa tulime badala ya kutegemea korosho peke yake. Kunawatu walilima ekari ishirini, hawaiwezi kuvuna bila vibarua. Nadhani ni muda wa serikali wakututafutia masoko, maana sisi tumetimiza wajibu wetu tayari," alisema Nzige mwenye ekari nne za zao hilo.
Mkulima mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Ali Nasoro, alisema kukosekana kwa soko la uhakika la zao hilo kumesababisha mitafaruku katika jamii. Kwamadai kuwa baadhi ya wakulima walikopa pembejeo na mahitaji mengine kwa matarajio ya kulipa kwakutumia fedha ambazo zingetokana na mauzo ya zao hilo.
Alisema licha ya bei kuwa ndogo lakini kwa sasa hazinunuliwi kabisa. Huku alitabiri kuwa kutakuwa kesi nyingi za madai. Kwasababu watu wengi watashitakiana.
"Kunawatu walikopa salfa, wengine waliwaweka vibarua wawafayatulie tofali, sasa bei ya mbaazi ndiyo hiyo, tutarajie kesi na magomvi," alisema Ali.
Mkulima huyo alisema atavuna zitakazotosha kwa mboga tu. Nyingine ataziacha ziozee shambani. Kwamadai kwamba hataweza kuvuna shamba lote bila ya vibarua.
Maelezo ya Ali yaliungwa mkono na mzee Hussein Haji, ambae pia alisema hatavuna mbaazi zote zilizo po shambani mwake. Mzee Hussein alitoa wito kwa serikali kulitafutia soko zao hilo. Huku akilinganisha bei ya shilingi 250 nisawa na bei ya kikombe kimoja cha chai au ndoo moja ya maji.
Mmoja wawakulima aliyejiita mkulima mkubwa, ambae hakutaka jina lake liandikwe. Alisema aliweka nguvu kubwa kwenye kilimo cha zao hilo. Kwakulima ekari 25, ambazo hataweza kuvuna. Akiweka wazi kuwa hayupo tayari kuendelea kupoteza fedha kwa kuweka vibarua. Badala yake ataziacha ziozee shambani.
Zao kwa msimu wa 2015/2016, bei ya chini lilikuwa linanunuliwa kwa shilingi 800 kwa kila kilo moja

No comments:
Post a Comment