Raphael Daudi.
Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema alitarajia kumpokea kiungo huyo jana baada ya viongozi kumtaarifu kuwa Raphael yupo njiani akielekea kambini huko.
Saleh alisema kiungo atajiunga na kambi hiyo baada ya kupata taarifa za Raphael kumalizana na viongozi wa timu hiyo katika mkataba wake aliousaini wa miaka miwili.
“Kambi huku Morogoro inaendelea vizuri na leo (jana) ninatarajia kumpokea Raphael kwa ajili ya kujiunga na kikosi chetu kinachojiandaa na msimu ujao.
“Nitampokea Raphael baada ya kupata taarifa kutoka kwa viongozi wakinitaarifu kuwa wamemalizana na kiungo huyo na yupo safarini akielekea huku kambini.
“Kama unavyojua Raphael tulikuwa tumemalizana muda mrefu na michuano ya Cosafa iliyofanyika nchini Afrika akiwa na Taifa Stars ndiyo ilimchelewesha kujiunga na timu,” alisema Saleh.
No comments:
Post a Comment