Wednesday, June 14, 2017

KASEJA KUHUSU KUCHEZA TIMU YA TAIFA


Juma Kaseja ni miongoni mwa magolikipa waliopata kujizolea umaarufu kwenye soka la Bongo kutokana na umahiri wake wa kulinda nyavu zake zisitikiswe.

Golikipa huyo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Kagera Sugar amevunja ukimya na kusema bado ana ndoto siku moja arudi kuitumikia timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kaseja amesema hajawahi kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa kama baadhi ya watu wanavyodai bali amekuwa haitwi kwenye kikosi cha Stars kwa ajili ya mechi mbalimbali ambazo Stars inacheza.

“Nina ndoto za kurudi timu ya taifa na uwezo huo ninao wa kucheza timu ya taifa. Sijawahi kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa na ninaamini uwezo ninao wa kucheza timu ya taifa.”

“Shida ya mpira wa Tanzania ni huyu aliwahi kugombana na nani au hyu aliwahi kufanya kosa mwalimu akiwa nani, kwa hiyo linachukuliwa kosa la kule anavishwa mwalimu mwingine kwamba huyu aliwahi kufanya hivi.”

“Tusiwalaumu makocha wazawa tuwape support kwa sababu wanateuliwa lakini wanafanya kazi kwenye mazingira magumu mno, kama wazungu wanaweza kuingiliwa hadi katika majukumu yao vuta picha hawa wazawa itakuwaje.”

“Tatizo langu kwenye timu ya taifa lilianza Uganda tukiwa na Kim nadhani kwenye kombe la Challenge, tukaambiwa tufungulie kwa sababu ya game. Mimi nikawaambia ilianza dini halafu ndio ukaja mpira na vitu vingine kwa hiyo mimi nitafunga siwezi kufungua kama Mungu katuandikia tutashinda mechi hii basi tutashinda na kama katuandikia kufungwa tutafungwa. Watu wengine wakafungua mimi niakaendelea kufunga pamoja na Kiemba ambaye na yeye alikataa kufungua.”

“Tulivyocheza ile mechi tukafungwa, ile ndio watu wanaichukulia kwamba mwalimu aliwaita watu na Juma akiwa nahodha akashindwa kuwashauri wenzeke kutekeleza matakwa ya mwalimu ili timu ipate matokeo.”

Kaseja alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi January 2017 katika msimu uliomalizika hivi karibuni baada ya kufanya vizuri na kuisaidia timu ya Kagera Sugar kushinda pointi tisa katika mwezi huo kufuatia kushinda michezo mitatu.

Pia alitajwa kwenye orodha ya magolikipa watatu waliokuwa wakiwania tuzo ya golikipa bora wa msimu 2016/2017 tuzo iliyochukuliwa na Aishi Manula aliyekuwa akiidakia Azam FC.

No comments:

Post a Comment