Monday, May 29, 2017

RAIS PUTIN NA MACRON KUJADILI VIPAUMBELE VYAO


Rais wa ufaransa Emmanuel Macron amemwambia mshirika wake wa Urusi Vladimir Putin kuwa kipaumbele chao kinapaswa kuwa ni kutafuta suluhu ya kisisasa huko Syria ili kuondokana na vitisho vya kigaidi. Katika mkutano wao uliofanyika katika ikulu ya Versailles karibu na mji wa Paris, wawili hao walikubaliana kurudisha mazungumzo na Ujerumani juu ya Ukraine.

Rais Putin ameomba kuondolewa vikwazo kwa Urusi , akisema kuwa havisaidii chochote.
Vilevile rais Putin amekataa kuhusika kwa Urusi katika uchaguzi wa Ufaransa uliomalizika hivi karibuni, amesema kuwa kukutana kwake na mshindani wa Macron Bi Marine Le Pen hakukuwa na uhusiano wowote na matokeo ya Uchaguzi.

Macron alijaribu kutoa ufafanuzi wa maamuzi yake ya kufungia vyombo viwili vya Habari kutoka urusi akidai kuwa vinasambaa habari za uongo kuhusu yeye kipindi cha Kampeni.

No comments:

Post a Comment