Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani
Korogwe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameombwa kupeleka msaada wa vyakula, nguo na dawa kwa wakazi wa vijiji saba vilivyokumbwa na mafuriko wilayani hapa.Ombi hilo limetolewa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (Profesa Majimarefu) baada ya kutembelea Kijiji cha Mkumbara ambacho ni miongoni mwa vilivyokumbwa na mafuriko.
Mbunge huyo amesema kutokana na athari zilizojitokeza kuna ulazima wa ofisi ya waziri mkuu kupitia kitengo cha maafa kutoa msaada kwa waathirika wa mafuriko hayo.
"Nitashangaa kama Serikali haitaleta msaada wa vyakula, dawa na nguo huku. Nitaona hata huu ubunge hauna maana kama wananchi wataachwa bila kupewa msaada kutokana na maafa haya,” amesema.
No comments:
Post a Comment