Wednesday, May 17, 2017

KIKWETE APEWA CHEO UN

Rais mstaafu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amechaguliwa  kuwa mwenyekiti mwenza wa  Baraza la Kimataifa  la Wakimbizi.

Rais Kikwete amechaguliwa kushika wadhfa huo wakati akiwa bado ni Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya (High-Level Panel on Global Responses to Health Crises). Itakumbukwa kuwa mwaka juzi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alimteua  Rais Kikwete kushika wadhfa huo.

Na sasa amekuwa tena kiongozi wa ngazi ya juu wa baraza hilo la kimataifa, ambapo katika nafasi hiyo  atakuwa na wenyeviti  wenza ambao ni Hina Jilani kutoka Pakistan na Rita Sussmuth kutoka Germany.

Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza  baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1951 ni Lloyd Axworthy kutoka Canada.

No comments:

Post a Comment