Friday, July 28, 2017

NJAA YAKUMBA YEMEN,WATI MILION 7 WAKABILIWA NA BAA LA NJAA


Wafanyakazi wa mashirika ya misaada waliopo nchini Yeman wamesema kuwa watu wapatao million saba wanakabiliwa na baa la njaa nchini humo.

Shirika la chakula Duniani WFP limesema kuwa asilimia 60 ya raia wa taifa hilo hawana uhakika wa kupata mlo na kushindwa kujua kuwa chakula kitatoka wapi.

Hali hii imesababishwa na mapigano ya miaka miwili kati serikali ya Yemen na waasi wa Houthi hali ilisababisha hali mbaya katika huduma za kibinadamu.

Janga hilo la njaa pia linachangiwa na kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu ulioathiri mamia kwa maelfu ya raia, ikiwa ni pamoja na kusababisha vifo kwa watu 200.

Madaktari wameiambia BBC kutoka mjini Yemen kuwa taifa hilo lipo hatarini kupoteza watoto nusu million kutokana na ugonjwa wa utapia mlo.

No comments:

Post a Comment