Mbunge
wa Nzega mjini, Hussein Mohamed Bashe amesikitishwa na Serikali ya
Kenya kuweka zuio la kuingiza mitungi ya gesi inayotoka Tanzania kwa
kusema ni vizuri nchi hiyo ikaheshimu mikataba ya 'East African
Community (EAC)' .
Bashe
amesema hayo baada ya serikali ya Kenya kupitia Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Andrew Kamau kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya
kupikia kutoka Tanzania kupitia mipaka ya nchi hiyo.
"Serikali
ya Kenya imezuia gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tanzania
kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu 'EAC treaty common'......Dar es
salaam 'port and Cost' ya gesi inayotoka Tanzania ndiyo 'competetive
edge' ya makampuni ya Tanzania dhidi ya yale ya Kenya uamuzi huu si
sawa". Ameandika Bashe kupitia ukurasa wake wa twitter.
Serekali ya Kenya imezuia Gesi za matumizi ya nyumbani zinazotoka Tz kuingia Kenya ni vizuri Kenya ikaheshimu EAC treaty "Common mkt"— Hussein M Bashe (@HusseinBashe) April 26, 2017
Quality ,Dar port and Cost ya Gesi inayotoka Tz ndo competitive edge ya Ma kampuni ya Tz dhidi ya Yale ya kenya uamuzi huu si sawa.— Hussein M Bashe (@HusseinBashe) April 26, 2017
No comments:
Post a Comment