Tuesday, March 21, 2017

MVUA YASABABISHA MAFURIKO MKOANI MOROGORO



Mvua kubwa zilizonyesha katika milima ya Mguruwandege kata ya Lukobe manispaa ya Morogoro zimesababisha mafuriko katika mtaa wa Mgudeni Kihonda ambapo baadhi ya nyuma na maduka vimezingirwa na maji huku kituo cha Upendo Clinic kikijaa maji na kupelekea uharibifu wa dawa na vifaa tiba.

Wakizungumza kwa uchungu wakazi hao wamelalamikia barabara ya Mazimbu Lukobe kukosa mifereji ya kupitisha maji huku kukiwekwa kifusi cha mchanga bila kusambazwa jambo lililochangia kusababisha maji kujaa kwenye kakazi ya watu.

Upendo clinic ni moja ya nyumba zilizoathirika na mafuriko hayo ambapo mkurugenzi wa kituo hicho Daktari Peter Peter ameeleza kusikitishwa na mafuriko hayo ambayo yamemsababishia hasara kubwa sana.

Kwa upande wake mhandisi wa manispaa ya Morogoro mhandisi  Godwine Mpinzire ameeleza kilichosababisha ujenzi wa barabara hiyo kusimama ni mvua zinazonyesha na kwamba usambazaji wa kifusi kilichopo katika barabara hiyo ni pale mvua zitakapokoma.

No comments:

Post a Comment