Shirikisho
la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limetoa siku 14 kwa Serikali
kurejesha fedha za makato ya mikopo ya asilimia 15 zilizokatwa
kikamakosa kupitia Bodi ya Mikopo, likisema sera inayotumika imejaa
utata.
Akizungumza
jana Dar es Salaam, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, alisema Serikali
lazima irekebishe sheria hiyo ya Bodi ya Mikopo kupitia Wizara ya
Elimu, Teknolojia na Ufundi Stadi kutokana na kuwajumuisha wafanyakazi
wote katika makato ya asilimia 15 wakati imetungwa hivi karibuni.
Nyamhokya
alisema kuwa wakati sheria hiyo inatungwa, baadhi ya wafanyakazi
walikwishaingia makubaliano mengine ya kukatwa asilimia 8 katika
mishahara yao.
Alisema wamesikitishwa na hatua hiyo ya Serikali, ingawa wanaamini haitalifumbia macho suala hilo.
Aidha
Nyamhokya alisema kuna milolongo mingi ya makato katika mishahara ya
wafanyakazi ambayo ni zaidi ya asilimia 57, huku pia mazingira ya
kufanyia kazi yakiendelea kuwa magumu na Serikali ikishindwa kuongeza
mishahara wala kuwapandisha vyeo kwa muda mrefu.
Aidha
alisema kwa kawaida mtumishi mwenye mkopo serikalini analipa kwa
makubaliano maalumu, lakini mtindo wa bodi hiyo kukusanya fedha za
wanufaika kabla ya kuanza kwa sheria husika kumeleta athari kwa watu
wengine.
No comments:
Post a Comment