Mgogoro
wa Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF umeendelea kufukuta ambapo
Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Vyama vya
Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara,
Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad
baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa Mwenyekiti wake kwenda Ofisi kuu
Buguruni kwa zaidi ya mara nne
Prof.
Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja
na wafuasi wa chama hicho, amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda
Makao Makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia
mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya
chama hicho
Aidha,
Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurugenzi kutoka Zanzibar akiwemo
Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Omar Ali Salehe
Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdalah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha
na Uchumi, Pavu Juma Abdallah - Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima
Katibu Mtendaji JUVICUF pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi
na Usalama CUF wote kutoka Zanzibar.
Chama
cha Wananchi CUF kimekumbwa na Mgogoro wa uongozi tangu Prof. Lipumba
alipotangaza kujiuzulu uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015, ambapo baadaye alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu
ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya CUF bara na CUF
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment