YANGA
imeshindwa kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya
kutolewa na Zanaco ya Zambia kutokana na sare mbili mfululizo.
Sare
ya kwanza ilikuwa ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam, hii ndiyo iliyoitoa
Yanga baada ya sare ya bila mabao mjini Lusaka. Zanaco wamevuka kwa
faida ya bao la ugenini.
Wakati
Yanga inatolewa, lazima kukubali kwamba yale malengo ya kumuondoa Kocha
Hans van Der Pluijm na kumchukua Mzambia, George Lwandamina yamefeli.
Yamefeli
kwa kuwa kwa viwango vya Tanzania, Pluijm raia wa Uholanzi alifiti na
kupata mafanikio yote. Yanga ilitaka kocha ambaye ataipeleka Ligi ya
Mabingwa Afrika mbele zaidi na si kurudi katika Kombe la Shirikisho.
Lakini leo wametumbukia katika shimo alilopita Pluijm, msimu uliopita.
Yanga
walitaka kwenda zaidi ya pale alipoishia Pluijm katika Ligi ya
Mabingwa. Hawakutaka kuangukia tena katika Kombe la Shirikisho ambalo
msimu uliopita walikuwa na mafanikio kwa kiwango chao au chetu.
Pluijm
alishindwa Ligi ya Mabingwa Afrika, akarejea Kombe la Shirikisho na
kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nane bora ambako ndiyo ulikuwa mwisho
wa Yanga.
Hakika
msimu uliopita kwa Yanga haukuwa haba. Pamoja na kushinda ubingwa wa
Bara, Kombe la Shirikisho lakini walikwenda hadi nane bora ya Kombe la
Shirikisho kwa mara ya kwanza.
Kutaka
zaidi si jambo baya hasa kwa mtu ambaye ni mwenye malengo. Hauwezi
kuwalaumu Yanga kumleta Lwandamina kama sehemu ya kuangalia kwenda mbele
zaidi kwa kuwa walikuwa katika kujaribu.
Lazima
wote tukubali kwamba Yanga walikuwa na nia nzuri kwa ajili ya klabu
yao. Lakini si kila unalopanga huwa lazima liwe unavyotaka kwa kuwa
unakutana na watu ambao pia wanapanga na wanakuwa na malengo yao.
Katika
mipangilio ya malengo unaweza kuteleza na kutoa nafasi kwa wenzako.
Huenda kuna wengine waliteleza msimu uliopita na Yanga ikafanikiwa.
Lwandamina
anapaswa kuelezwa ukweli kwamba amefeli lile lengo hasa la kutaka
kuiona Yanga inavuka kutoka katika nane bora ya Kombe la Shirikisho hadi
Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lakini
anapaswa kupewa sapoti katika Kombe la Shirikisho kwa kuwa Yanga
wanapaswa kukubaliana na kilichotokea kwamba bado wanashiriki michuano
ya kimataifa. Wao ndiyo wawakilishi wa mashabiki na wanachama wao na
wawakilishi wa taifa la Tanzania.
Hivyo
Lwandamina sasa anapaswa kuwa na plani mpya na ya uhakika kuhusiana na
michuano ya Kombe la Shirikisho na si wakati mzuri kuanza kuwaza
kuhusiana na walivyotolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa
kifupi au hali halisi ni kwamba, Lwandamina ana deni, kwani Pluijm
aliyepita kabla yake, alifanya vema na kufika hatua ya juu zaidi katika
michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho. Hivyo kwa kuwa ameangukia huko, ni
lazima kufanya juhudi na maarifa na kuhakikisha anafikia pale alipokuwa
kocha huyo aliyepita na ikiwezekana kuvuka pale.
Kama
kocha mzoefu na aliyepata mafanikio, lazima ajue tofauti ya Yanga na
Zesco kwa kuwa Yanga ni timu ya wanachama na si timu ya kampuni. Pia ina
presha kubwa sana ukilinganisha na Zesco ambayo inamilikiwa na Shirika
la Umeme la Zambia.
Kingine
kikubwa ni kwa mashabiki na wanachama wa Yanga wenyewe. Nao wanapaswa
kujua kwamba kama alifanikiwa akiwa na Zesco, basi inawezekana na sapoti
kutoka kwa wanachama au mashabiki wao wachache na viongozi, ilikuwa
kubwa sana.
Hivyo,
kwa kipindi hiki badala ya kuendelea kumsakama. Kuendelea kumuona kama
ni mtu mbaya sana, basi iko haja ya kumuunga mkono ili aonyeshe au awape
alichonacho na vizuri kama atashindwa huku wakiwa wakimuunga mkono.
No comments:
Post a Comment