Taarifa hizo zinadai kuwa ofisi za Clouds Media Group zilizopo Mikocheni B Dar es Salaam, zilivamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Usiku wa Machi 17 mwaka huu.
Taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa bado zinaenda mbali zaidi na kudai kuwa, RC Makonda alikuwa ameambatana na Askari wakiwa na silaha ambapo aliwashinikiza watangazaji wa kipindi cha De Weekend Chat Show kurusha mkanda wa video aliorekodiwa mwanamke mmoja na anayedai kuwa alizaa na Askofu Gwajima.
Waziri Nape amesema kuwa yeye kama kiongozi mwenye dhamana na tasnia ya habari, atakwenda ili afahamu ukweli wa mambo kuhusu hasa kilichotokea.……
“march 20
asubuhi kama Waziri Mwenye dhamana na HABARI nitatembelea Clouds Media
kujua kilichotokea. Nawaomba sana wanahabari nchini KUTULIA kwasasa”
No comments:
Post a Comment