Mbunge
wa Singida Magharibi Elibariki Kingu ameibuka na kuweka wazi kuwa yuko
tayari kufukuzwa ndani ya chama chake cha CCM kwa kupinga uhalali wa
elimu ya Mkuu wa Mkoa wa dar es Salaam.
Katika
taarifa yake aliyoitoa leo, Kingu amesema anasikitishwa na ukimya
uliotanda miongo mwa wanachama wa CCM kwa hofu ya kufukuzwa uanachama na
kuacha Rais Magufuli akisemwa vibaya kila kona ya nchi kwa sababu ya
kiongozi mmoja ambaye uhalali wa elimu yake unatiliwa shaka.
"Najua
hofu mliyonayo watanzania juu ya huyu RC. Ikiwa mamlaka zitaendelea
kufumbia macho. Mimi Elibariki Immanuel Kingu mbunge wa CCM nitakuwa wa
kwanza kufukuzwa CCM kama kupinga matendo maovu ya RC huyu itaonekana ni
usaliti kwa nchi. Haiwezekani Rais wetu atukanwe kila kona kwa matendo
ya mtu huyu. Wana CCM ukimya wetu kwenye hili halikubaliki". Amesema Kingu.
Kingu
amekieleza kituo cha EATV kuwa anakerwa na kusikitishwa na kelele
zinazoendelea mitandaoni kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
kughushi vyeti vyake vya taaluma huku matusi na kejeli zikipelekwa kwa
Rais, na bado wana CCM wako kimya.
Pia ameonesha kukerwa na kile alichokiita matendo yanayokiuka utawala wa sheria yanayofanywa na mkuu huyo wa mkoa.
"Naomba
sasa niweke kumbukumbu sawa najua mnamchafua kila anayempinga RC huyu
kwa matendo yake ambayo yanakiuka utawala bora. Naomba niwe wa kwanza
kufukuzwa CCM kwa kumpinga RC Makonda"
No comments:
Post a Comment