Wednesday, March 1, 2017

LEICESTER YAFANYA MAZUNGUMZO NA ALIYEKUWA KOCHA WA UINGEREZA ROY HODGSON


Klabu ya Uingereza ya Leicester imefanya mazungumzo na aliyekuwa kocha wa taifa la Uingereza Roy Hodgson kuhusu kurithi pengo lililoachwa na Claudio Ranieri aliyepigwa kalamu.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Roy ni miongoni mwa mameneja waliofanya majadiliano na wakuu wa timu hiyo.

Na kaimu mkufunzi Craig Shakespeare huenda akaendelea kuifunza timu hiyo hadi mwisho wa msimu iwapo matokeo yataendelea kuimarika.

Ranieri alifutwa kazi mnamo tarehe 23 mwezi Februari ,miezi tisa baada ya kushinda taji la ligi na kikosi hicho.

Mechi ya kwanza chini ya usimamizi wa Shakespear ilitoa majibu ya ushindi wa 3-1 dhidi ya liverpool siku ya Jumatatu.

Beki Danny Simpson alisema kuwa Shakespeare “ni kocha mzuri sana”.

Aliongeza, “Alituambia kwa urahisi kile anachotaka kufanya , na ilikuwa rahisi .Tumefanya hivyo na tunatumai kwamba tutaendelea hivyo.

No comments:

Post a Comment