Thursday, March 16, 2017

JAJI WA HAWAII AMEZUIA MARUFUKU MPYA YA RAIS TRUMP KUINGIA MAREKANI


Jaji wa Hawaii amezuia marufuku mpya ya kuingia Marekani iliyowekwa na Rais Donald Trump, saa chache kabla ya kutakiwa kuanza kufanya kazi, Alhamis hii.

Jaji Derrick Watson amesema kuna ushahidi wenye uwalakini kuhusu madai ya serikali kuwa marufuku hiyo ni kwaajili ya usalama wa nchi.

Amri hiyo ingefanya kuwepo marufuku ya siku 90 kwa raia kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani na siku 120 za kuzuia wakimbizi.

Trump anasisitiza kuwa hatua hiyo ni kwaajili ya kuzuia magaidi kuingia nchini Marekani lakini wakosoaji wanaielezea kama ya kibaguzi. Awali, marufuku hiyo ilipingwa na jaji wa Seattle.

Akizungumza kwenye mkutano huko Nashville, Tennessee, Jumatano jioni, Trump alisema hatua hiyo ya jaji wa Hawaii inaifanya Marekani ionekane dhaifu.

Alisema ataendelea kuipigania na kwamba ,”We’re going to win.”

No comments:

Post a Comment